JE ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA ? - MULTISKILLS CONSULTANCY

Latest

business & management consultancy

Monday, May 29, 2017

JE ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA ?

JE ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA ?




Kuna huu msemo wa siku nying unaosema "Elimu ni ufunguo wa maisha" Kama ni kweli elimu mi ufunguo wa maiha basi kuna nyumba inaitwa MAISHA. Pamoja kuwepo kwa nyumba hii nadhani wengi hatujaweza kufikia na kufungua ili kupakua maisha yaliyoko humo ndani ya nyumba hii. pamoja na kuwa bado kiwango cha wasomi nchini ni kidogo kulinganisha na wingi wa watu tulionao basi hata hawa wachache tuliyomo bado hatujafikia nyumba MAISHA. Unafikiri kwanini watu wamesoma na bado maisha yanawapiga chenga? Najaribu kujiuliza baadhi ya maswali :Je tatizo ni mfumo wa elimu yetu?Je tatizo ni wenye elimu? Au tatizo ni watoa elimu (wakufunzi)? Kwa mtazamo wangu nadhani tatizo liko kwa waliosoma. Mojawapo ya sifa kubwa ya mtu aliyesoma ni kuogopa kudhubutu kupoteza.(Risk averses). Tatizo lingine la mtu aliyesoma ni kukukariri kuwa ukimaliza shule lazima uajiriwe, pamoja na mtazamo huo kutokuwa mbaya lakini lingine linalowakumba ni kuingia kwenye dhambi ya kulalamika na kunungunikia serikali. watu tuliosoma tuna tabia ya kulalamika sana badala ya kutafutanjia mbadala. Watu tuliosoma tumefaulu vizuri vyeti vinapendeza sana lakini tumefeli kumudu maisha au kusaidia watu wasio soma kuamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Ni kweli elimu ni ufunguo wa maisha , mimi sina ubishi juu ya hili hata kidogo. Tukisema elimu ni ufunguo wa maisha ni kweli kwa sababu zifuatazo: Kabisa elimu (kwenda shule) ndikokuliko anza kukukutanisha na watoto wenzako na kuanza kushirikiana tabia na kujifunza tofauti ya maisha ya baba na mama yako, Pili baada ya kwenda sekonndari ndipo ukaanza kukutana na watu wa makabila tofauti tofauti na ukajifunza zaidi ,Tatu ulivyoenda chuo ukazidi kukutana na watu wazima kama wewe na kujifunza zaidi tabia , miendendo na uweledi au utaalamu na katika kujifunza huko ulikutana na simulizi mabali mabali kutoka kwa wakufunzi na wanachuo wenzako. Mpaka hapo umepata ufunguo wa kukutana na watu mbalimbali na kujua tamaduni mabali mabali na hulka za watu mabali. Huo ni ufunguo mojawapo. Lakini n kubw zaidiumesoma vitabu mbali mbali za wataalamu walio hai na wengine waliokufa na ukapata ujuzi waliotumia kumudu maisha . Kufikia hapo nadhani huna ubisha kuwa elimu haijakuwa ufunguo wa maisha. Sasa ufunguo  mkubwa ni utaalam ulio pata shuleni au chuoni , je huu unatumiaje kufungulia nyumba inayoitwa maisha? Nyumba maisha ina tafsiri nyingi kwa msomi, inaweza kuwa mazingira yaliyokuzunguka , inaweza kuwa kituo chako cha kazi, inaweza kuwa siasa, inaweza pia kuwa mwenendo wako kwa ujumla. Elimu ni ufunguo wa maisha hakuna ubishi, acha kulalamikia serkali, acha kujilaumu, acha kungunika, acha kulalamikia ukosefu wa mtaji. Tumia elimu kukabili a kutatua  changamoto.

3 comments:

  1. KAMA ELMU NI UFUNGUO UMEFUNGUA MLANGO UPI?

    Tumeona kuwa elimu ni ufunguo wa maisha kwani inaanza kukufungulia mlanago wa kukutana na watoto amabao sio Ndugu wala hakuna uko Nao na hatimaye kukutanisha na way mbali mbali kwenye upeo tofauti tofauti hadi kukutanisha na wataalamu watakaokupa utaalamu wa kukufanya uwe na ujuzi au utaalamu ambayo ndiyo hasa ufunguo wa kuweza kukufungulia Nyumba maisha.He Nyumba inayoitwa maisha ni IPI?Nyumba maisha ni mahali popote utakapokuwa ,ni mazingira yeyote utakayokuwa,uwe kazini uwe nyumbani au mahali popote hakikisha unatumia elimu yako kupambanua mazingira,hakikisha unatafuta changamoto zilizoko kwenye mazingira uliyoko na kwa kutambua changamoto tumia elimu au ujuzi uliyonao kugeuza changamoto kuwa fursa na chanzo cha kipato.Kwa kufanya hivyo utakuwa umefungua Nyumba inayoitwa maisha.Ukitaka kuonana ufunguo wako haufanyi Kazi anza kulalamikia mazingira uliyoko au anza kulaumu watu wanaokuzunguka au kulaumu viongozi au serikali! Hakikisha unafanya mambo kwa mtazamo chanya na sio hasi wala lawama.Ukiona unaanza kulaumu mazingira na watu au serikali Juma karibu utapoteza mwelekeo na ufunguo wako(elimu).Kama unaona elimu uliyonayo haendani na mazingira uliyoko na fursa unaziona basi tafuta elimu inayofuatana na mazingira uliyopo! Mfano kuna MTU mmoja alisomea mambo yabkuunga vyuma lakini akawa kijijini na mule hakuna vyuma wala karakana akakwa hajui pa kuanzia wala pa kutumia ujuzi alionao! Mwisho akaamu a kuchimba bwawa na kuvuna Maji ya mvua kwa msimu na pole pole aliyahifadhi hayo Maji na kuanzia kuyatumia wskati wakiangazi kuotesha mboga na niche michache ya migomba.Wskati wakiangazinkumekauka kabisa alianza kuwauzia watu mboga na kufunga wlndege na akaanza kutengenza kipato na mwisho alibadili fikra na mtazamo wa watu juu yake. Katika mazingira hayo alianza kujifunza Kilimo cha mboga mboga na kuweza kuwa utaalamu wa mboga na matunda na hatimaye akawa mshauri mkubwa wa lishe na Kilimo mboga mboga.Acha kulalamika kuwa mbunifu,!!

    ReplyDelete
  2. UFUNGUO WA MAISHA UMEFUNGULIA MLANGO UPI?

    Kama yulivyoona kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na unaweza kuwa una elimu lakini huoni mlango wa kufungulia.Sababu kubwa ni kwamba pengine ulichukua ufunguo ambayo hujui kutumia au mpaka uone MLANGO wa kufungulia kunahitaji tufanye Kazi ya ziada! Kuna watu wamesoma elimu wasioipenda au wasiojua wapi pa kutumia ,wamesoma tu kwa msukumo wa wazazi au marafiki lakini pengine hawapendi au walijikuta tu wamepangiwa kusoma na serikali! Ukitaka ufunguo wako ufungue kila MLANGO basi Fanya au soma kitu kinachotoka moyoni kwako na sio vinginevyo.Kwa kufanya hivyo utakuwa umefungulia elimu yako MLANGO uliosahihi!Ukitaka kufanikiwa katika maisha Fanya mambo yafuatayo: Kwanza hakikisha una Imani sahihi juu ya Mungu unaye kwanini,pili hakikisha unakaa Katibu na watu waliofanikiwa kwa kutumia elimu yao inayofanana na yako,tatu wadadasi mbinu au kanuni walizofuata kufanikuwa,tatu hakikisha hujidharau mwenyewe,nne usikubali mazingira yakutawale,tano hakikisha neno sitaweza haliko akilini kwako,sita kaa mbali na walioshindwa na wakatisha tamaa,saba sikiliza nafasi yako katika kutenda Yale unayofikiri, Nane usiache kujifunza kwa tusafiri au kusoma Vitabu,Tisa jifunze kutoka baada ya kufanikiwa,kumi mafanikio yasikutenge na watu wala Mungu. Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanweza kukufanya ufunguo wako wa maisha tufanye Kazi vizuri! Kwa kufuata hizo kanuni ufunguo wako wa maisha utafungua kila MLANGO wa mafanikio.Pia jifunze kutokuwa mbinafsi.Nakutakia mafanikio mema na uwe na wskati mwema wa kujifunza

    ReplyDelete
    Replies
    1. KAMA ELIMU NI UFUNGUO KWANINI WATU WENGINEWATUMIE UFUNGUO WAKO?

      Watu wengine tuliosoma hatupendi kutumia elimu kwa manufaa yetu isipokuwa tunakimbilia kutimiza ndiyo na maono ya watu wengine! Kwa lugha nyingine tunatumia elimu yetu kuwafungulia wengine milango yako ya naisha.Fikiri unasoma unawaza tu kutumia na watu wabunifu tena wasio na utaalamu ulio Nao!Sikiliza ajira ni njia sahihi ya kusikia umasikini wa kipato! Na ajira ni ajira tu hata ubadilishe mwajiri ni sawa na kubadili njia ya unayotumia kusafiria kuelekea katika umasikini wa kipato!Sina maana ya kuchukua ajira ila tunapoajiriwa tuache kuwaza mshahara kuongezeka tu,fikiria jinsi ya kuongea kipato na njia halali za kupata kipato! "Employment is never certain" Ukitengeneza milango yako ya hela umetengeneza kofuli LA Nyumba yako ambayo ufunguo unajua kutengeza mwenyewe pia hivyo hutakaa ushindwe kufunga! Amka acha kufungulia watu maisha fungua ya kwako mwenyewe! Tuma elimu kwa manufaa yako na wengine!

      Delete