Matumizisahihiya elimunikwa ajiliya kulitumikia Taifa lako,Uwe mzalishaji binafsi au umeajiriwa au unafanya chochote kile cha kukufanya uweze kuishi , yote ni kwa manufaa ya taifa lako.Elimu ni msingi wa maendeleo na ufanisi wa maisha. Elimu ni mwanga ,elimu ni njia pekee inayokupa ujasiri na uwezo wa kukutana na kuongea na watu wenye wadhifa mbali mbali. Kuna njia nyingine chache za kukufanya ufikie maendeleo ya kweli na ufanisi wa maisha lakini elimu bado ndiyo njia pekee na iliyo kubwa ya kufikia mafanikio yenye tija. Kuna msemo wa zamani sana unaosema " Kosa mali pata akili" Huu msemo una ukweli usio pingika kwani ukipata mali bila kupata akili(elimu) mali hivyo hutaweza kupangilia ipasavyo. Katika mtiririko wa kutafuta mafanikio ni Vizuri kuwa na mpangilio huu: Tafuta elimu kwanza, alafu tafuta mali na mwisho tafuta majukumu ya kutumia mali. Ukitafuta elimu alafu mali utawea kupangilia uzalizashaji na utoaji huduma kwa maana ya kutumia elimu
Ukianza kutumia elimu kutoa huduma au kuzalisha mali ni dhaihirikuwa utaweza kusimamia hicho unachokifanya kwa ufanisi mkubwa. utajua kuongoza watu walioko chini yako , utajua kusimamia matumizi sahihi ye fedha na uongozi uliyotuka . ukiwa na elimu utaweza kujua jinsi ya kuongea na wateja na watu wote wenye tija dhidiya maisha yako. Kutokuwa na elimu ni sawa na kutembea gizani na msituni.Kama unafanya kazi au unataka kufanya kazi yeyote inayohitaji kutumia elimu na huna elimu ni vizuriukawaajiriwatuwenye elimunautaalam wa unachotaka kufanya , usifanye jambo lolote kwa kubuni au kubahatisha, ni sawa na kujitibu kwa dawa yeyote bila kumuona daktari au kujua ugonjwa unaokusibu.
Ukishapata elimu na na kuanza kutumia kuzalisha au kutumia kutoa huduma kwa jamii au kwa wateja na kupata hela ndiyo sasa uanze kufikiri kuwa na majukumu ya familia na vitu vingine .Ni hatari sana kuanza majukumu bila kuwa na mali ,ni dhahiri kuwa majukumu yata kulemea na kukunyima uwezo wa kutengeneza mali na hatimaye utapata msongo wa mawazo na baadae kukuletea magonjwa .
No comments:
Post a Comment