ELIMU NA MAEND - MULTISKILLS CONSULTANCY

Latest

business & management consultancy

Wednesday, August 30, 2017

ELIMU NA MAEND

Elimu ni msingi wa meandeleo, nikisema elimu namaanisha elimu yeyote unayopata katika mazingira yeyote yawe mazingira rasmi au yasiyo rasmi. Mazingira rasmi ya elimu ni yale unayoenda kusoma darasani kwa muda maalum na kwa mpangilio maalum. Inahusisha wataalamu wa elimu na mbinu maalum za kukupatia elimu hiyo. Anayekufundisha elimu maalum na yeye karudishwa mbinu za kutoa elimu maalum. Elimu maalum inakupelekea kujifunza namna na hatua za kufuata katika kutekeleza jambo fulani. Mfano Daktari anafundishwa jinsi ya kutibu binadamu, askari anafundishwa jinsi ya kulinda raia na Mali zao, mwalimu anafundishwa namna ya kufundisha wanafunzi waweze kuelewa na kuweza kufanya kazi maalum.

Elimu isiyo rasmi hutokana na mazingira mtu anayoishi na mambo anayoyaona au changamoto anazokabiliana nazo. Kwa kukutana na changamoto na mazingira anayoishi mtu hujifunzi namna ya kuyamudu na kukabiliana na mazingira hayo, hii nayo ni elimu apatayo mtu kutokana na mazingira na changamoto za maisha anazokabiliana nayo! Ni mojawapo ya elimu muhimu sana kwani hujafanya mtu kuwa mbunifu na kufikiria zaidi ya yule anayjifunza elimu rasmi. Wajasiriamali wengi wametokea katika elimu isiyo rasmi. Watu wanaojifunza kupitia elimu isiyo rasmi huwa siyo waoga wa kudhubutu kuharibu mambo mbali mbali.

FAIDA ZA ELIMU ISIYO RASM
1.Humfanya mtu kujifunza jinsi ya kukabiliana na mazingira
2. Humfanya mtu kudhubutu kutenda mambo makubwa bila kujali nini kitatokea
3.Humpa mtu ujasiri wa kujifunza
4.Humpa mtu uhuru wa kufikiri na kuamua
5.Huweza kuibua wajasiriamali wanaoweza kuleta mchango makubwa katika maendeleo ya nchi
Elimu isyorasmi ndiyo chanzo kikubwa cha kuibua maendeleo kwani mtu anayefanya mambo kwa kutumia elimu isiyo rasmi mara nyingi huhitaji maelekezo machache kutoka Kwa wenye elimu rasmi.

No comments:

Post a Comment