Juhudi na maarifa ni shina la maendeleo. Unakumbuka hii ulikuwa ni salami za kumsalimia mwalimu akiingia darasani wskati nasoma shule ya msingi. Tulitamka haya maneno bila kujua maana yake. Ni miaka Mingi sana imepita lakini haya maneno yana maana kubwa sana.ukiwa na juhudi na unatumia maarifa kutafuta maendeleo lazima utafanikiwa ,Juhudi ni sehemu kubwa ya maendeleo juhudi inayoka moyoni na inatokana na nguvu ya maamuzi , juhudi ni msukumo wa ndani unaoyokana na kuchukua hata ya maendeleo uliopo na kutamani kwenda hatua nyingine bora zaidi. Kitendo cha kuchukua hatua ya maendeleo uliopo na kuamua kwenda nyingine bora zaidi inakupelekea kufanya maamuzi ya kutenda jambo LA kukuvusha hapo ulipo. Kitendo cha kufanya maamuzi kina kufanya kuwa na juhudi ya kutekeleza ulichoamua. Unapofanya maamuzi lazima utumie maarifa(elimu) aidha uliyonayo au uyatafute kwa kuhudhuria kipindi na semina au kusoma vitabuni au makala maalum au kutafuta ushauri kwa wataalamu wa eneo uliloamua kujikita. Kwa mfano mwanafunzi anayeamua kufanya vizuri katika somo fulani lazima afanye maamuzi ya kulipenda somo na pia kufanya maamuzi ya kujifunza kwa bidii lakini pamoja na kufanya maamuzi hayo lazima ampate mwalimu kwenye utaalamu wa hesabu. Hivyo kwa pia katika maendeleo lazima uwe na maamuzi ambayo huleta msukumo wa kufanya bidii na hatimaye utafute maarifa itakayo kuelekeza kufanya uliyoamua kufanya ."Juhudi na maarifa ni shins LA maendeleo shikamoo Ndugu mwalimu"Hiyo ndiyo ulikuwa salami yetu miaka hiyo ,ni salami yenye nguvu ,ni salami yenye maana ,ni salami yenye uzalendo ndani yake.Niambie ni nani anayetafuta maendeleo au uwekezaji katika Biashara yeyote bila kuwa na juhudi na kutumia maarifa? Hata wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini wanaanza kwanza juhudi za kuja nchini alafu wanajifunza mila na desturi zetu kwa kuwatumia wataalamu wetu au wazawa ndiyo waanze kuwekeza hela zako. Usianze kuwekeza hela au kuanzia Biashara bila kuwa na juhudi ya kufanisha hiyo Biashara. Usianze kuwekeza Biashara bila kupata maarifa(elimu) kuhusu hiyo Biashara .Ukiwa na juhudi na maarifa basi Biashara yako au uwekezaji wako utakuwa na shins imara.Karibu tushauriane
Wednesday, June 14, 2017
New
JUHUDI NA MAARIFA NI SHINA LA MAENDELEO
About MULTISKILSS CONSULTANCY COMPANY LIMITED
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment