UFUNGUO WA MAISHA UMEFUNGULIA MLANGO UPI? - MULTISKILLS CONSULTANCY

Latest

business & management consultancy

Friday, June 2, 2017

UFUNGUO WA MAISHA UMEFUNGULIA MLANGO UPI?

Kama yulivyoona kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na unaweza kuwa una elimu lakini huoni mlango wa kufungulia.Sababu kubwa ni kwamba pengine ulichukua ufunguo ambayo hujui kutumia au mpaka uone MLANGO wa kufungulia kunahitaji tufanye Kazi ya ziada! Kuna watu wamesoma elimu wasioipenda au wasiojua wapi pa kutumia ,wamesoma tu kwa msukumo wa wazazi au marafiki lakini pengine hawapendi au walijikuta tu wamepangiwa kusoma na serikali! Ukitaka ufunguo wako ufungue kila MLANGO basi Fanya au soma kitu kinachotoka moyoni kwako na sio vinginevyo.Kwa kufanya hivyo utakuwa umefungulia elimu yako MLANGO uliosahihi!Ukitaka kufanikiwa katika maisha Fanya mambo yafuatayo: Kwanza hakikisha una Imani sahihi juu ya Mungu unaye kwanini,pili hakikisha unakaa Katibu na watu waliofanikiwa kwa kutumia elimu yao inayofanana na yako,tatu wadadasi mbinu au kanuni walizofuata kufanikuwa,tatu hakikisha hujidharau mwenyewe,nne usikubali mazingira yakutawale,tano hakikisha neno sitaweza haliko akilini kwako,sita kaa mbali na walioshindwa na wakatisha tamaa,saba sikiliza nafasi yako katika kutenda Yale unayofikiri, Nane usiache kujifunza kwa tusafiri au kusoma Vitabu,Tisa jifunze kutoka baada ya kufanikiwa,kumi mafanikio yasikutenge na watu wala Mungu. Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanweza kukufanya ufunguo wako wa maisha tufanye Kazi vizuri! Kwa kufuata hizo kanuni ufunguo wako wa maisha utafungua kila MLANGO wa mafanikio.Pia jifunze kutokuwa mbinafsi.Nakutakia mafanikio mema na uwe na wskati mwema wa kujifunza

No comments:

Post a Comment