MSINGI WA ELIMU YAKO NI NINI - MULTISKILLS CONSULTANCY

Latest

business & management consultancy

Wednesday, June 21, 2017

MSINGI WA ELIMU YAKO NI NINI

Kuwa na elimu isiyo na msingi ni sawa kujenga nyumba isiyo na msingi. Elimu yenye msingi ni elimu inayotokana na wewe mwenyewe kuipenda na kujua mwisho wa elimu yako itakuletea matunda gani.
 Kusoma bila kujua unaenda wapi wapi ni sawa na kuendesha gari lisilo na taa usiku. kusoma bila kujua unataka kuwa nani ni sawa na kutembea safari isiyokuwa na mwekeo kwa lugha nyingine ni sawa na kuzurura. Mwisho wa siku elimu hiyo itakutesa na kukukera na ni rahisi kuwa na msongo wa mawazo .Ni muhimu kw wzazi na walezi kuzungumza na watoto wao vizuri kabla yakufanya maamuzi kwa au kuwafanyia maauzi ya kusomea utaalam fulani. Ni vizuri kumweleza mwanao kila elimu unayojua na pia kumpa muda mzuri wa kutafakari na kumruhusu akuulize maswali ya kutosha kuhusu ulichomweleza. Kama unaona kuwa mwanao anaweza kuwa maswali mengi kuhusu mwelekeo wa kitu anachotak kusomea mna huna mjibu ya kutosheleza ni vizuri utafute wataalum wa kozi husika ili wamwelekeze. Usimchaguluie mwanao au mtoto kitu cha kusoma kwa msing kuwa wewe unapenda hucho. Kumchagulia mwanao ni sawa na kumjengea msingi juu ya msingi wako, mwache ajenge msingi wake mwenyewe.
 Watu wengi wamejengewa misingi na wazazi wao au walezi wao na baada ya muda wazazi hawapo na na uimara wa msingi anajua wazazi . Kwa maana ya mzazi kama sehemu ya malezi unapaswa tu kumlea mtoto mpaka umri fulani hasa baada ya kuhitimu kidato cha nne unapaswa kuona anapenda nini na sio wewe unapenda nini. Ukishaona anapenda nini basi anza kumwelekeza nini cha kufanya na pia ujaribu kupima kwanini anapenda anachopenda , Kumruhusu mtoto ajenge msingi wake kuhusu utoto wake ni kumruhusu ajenge uwezo wa kufikiri na kufanya vizuri katika yale anayochagua kufanya. nimeona wazazi wengine wanalazimisha watoto kusoma alichosoma yeye mzazi , hii siyo sawa. 
 Jaribu kuona watu wengi wamejengewa misingi  amabayo imefika mahali hawawezi kufanya mamuzi ya kuendeleza misngi na hawajui mwisho wakujenga alichojengewa. Kuna umri ukifika Lzima ujengewe uwezo wa kuamuliwa na sio kuamuliwa. Kutokuwa na uwezo wa kuamua ni hatari sana na ni chanzo kikuu cha umasikini.

No comments:

Post a Comment